.
1st August, 2021
Mwaka mmoja baada ya Ktn News kuangazia madhila ya wasichana wa Karamajong katika eneo la Eastleigh hapa jijini Nairobi, wahanga hao wa ulanguzi wa binadamu wanaendelea kuhangaika. Kulingana na ripoti ya shirika la haki za watoto Afrika Mashariki (EACRN), wasichana takriban elfu tatu wako katika eneo la Eastleigh pekee. Kuzuka kwa virusi vya Covid-19 kumechangia pakubwa katika kunawiri kwa biashara ya ulanguzi wa binadamu. Anavyoarifu mwanahabari wetu Sirajurahman Abdullahi katika makala maalum ya Hadubini, wasichana hao bado wanalala nje huku wengi wao wakiripotiwa kunajisiwa, kupachikwa mimba na hata kujifungua barabarani.