Wenyeji wa Gatundu watatizwa na uvundo kutoka kwenye chumba cha kuifadhia mahiti
7th February, 2015
Wakazi wa mji wa Gatundu ulioko Kaunti ya Kiambu wamelalamikia uvundo mkali unaotoka kwenye hifadhi ya maiti ya hospitali ya wilaya ya Gatundu. Aidha, wasimamizi wa hospitali hiyo wanasema uvundo huo mara nyingi hutokana na maiti inayoletwa kwenye hifadhi hiyo na polisi ikiwa imeharibika. Wameongeza kuwa hifadhi hiyo haiwezi kuweka maiti zaidi ya kumi na nne.