×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Kivumbi chatarajiwa bungeni, Mswada wa Fedha wa 2023 ukijadiliwa

News

Kivumbi kinatarajiwa bungeni Alhamisi alasiri wakati Mswada wa Kifedha wa Mwaka 2023, utakapowasilishwa kusomwa kwa mara ya pili. Kisha wabunge watapata fursa ya kuujadili ambapo ubabe baina ya wabunge wa Kenya Kwanza na Azimio unatarajiwa kushuhudiwa.

Mswada huo wa Kifedha utawasilishwa na Kiongozi wa Wengi wa Bunge la Kitaifa Kimani Ichungwa ambaye jukumu lake kuu ni kuzisukuma ajenda za serikali bungeni.

Mara si moja viongozi wa upande wa wengi katika bunge wa kitaifa wamekuwa wakisisitiza kwamba watahakikisha kuwa Mswada huo unapitishwa. Ni wikendi hii ambapo Kiranja wa Wengi katika Bunge hilo la Kitaifa Silvanus Osoro, aliahidi kwmaba atahakikisha kuwa wabunge wote wa Kenya Kwanza wanahudhuria kikao cha leo. Hii hapa kauli hiyo.

Kikao cha leo kinatarajiwa kuwa cha kwanza kabisa kwa wabunge wa Kenya Kwanza kuonesha uwezo wao wa kujenga hoja na kutetea mipango ya serikali hasa ikizingatiwa pingamizi tele kutoka kwa upinzani.

Tayari uongozi wa Azimio umewataja wabunge wake kuupinga mswada huo huku ukisema unamwongezea mzigo Mkenya mlipa kodi kwa kuwa baadhi ya vipengele vyake vinapendekeza kuongezwa ushuru na matozo mengine.

Hata hivyo, inaonekana kuwa upande wa Kenya Kwanza u katika nafasi nzuri ya kutua ushindi, iwapo wabunge waliojitokeza kuunga mkono Kenya Kwanza baada ya uchaguzi wataunga mkono pia ajenda zake. Miongoni mwa waliohamia Kenya Kwanza ni wwaliokuwa wabunge wa Jubilee, UDM na Chama cha UPIA.

Kwa mfano lipo pendekezo la kuongeza mchango wa Wakenya kwenye mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kutoka asilimia 1.5 ya mishahara yao hadi asilimia 3 vilevile pendekezo la kuongeza ushuru kwenye bidhaa ya mafuta kutoka asilimia 8 hadi asilimia 16, ambayo yote yametajwa kumkandamiza mlipa ushuru.

Hata hivyo licha ya pingamizi hizo, Rais William Ruto aliendelea kupigia debe mapendekezo hayo akisema lengo kuu ni kutatua suala la mitaa ya mabanda nchini Slums.

Ikumbukwe mashirika kama vile Chama cha Watengenezaji Bidhaa KMA na viongozi wa makundi mbalimbali waliupinga mswada huo wakati wa kukusanya maoni, wakisema iwapo utapitishwa basi utawaongezea gharama kubwa ya uzalishaji na hata kuonya kuwa huenda wakahamia mataifa jirani iwapo utapitishwa jinsi ulivyo.

Haya yanajiir huku kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia na wanaharakati wengine wanne kupinga mswada huo ikitajwa kuwa ya dharura. Kwenye kesi hiyo Omtata ameorodhesha sababu kumi na tatu anazohisi kwamba mswada huo umekiuka katiba na kwamba unapaswa kufanyiwa marekebisho.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week