Wakenya wanatarajiwa kuendelea kugharamika zaidi kununua mafuta baada ya bidhaa hiyo kupanda katika tangazo la hivi karibuni la Mamlaka ya Kutathmini Bei ya Kawi ERPA.
Katika bei hiyo ambayo itatumika kwa mwezi mmoja ujao, bei ya petroli imepanda kwa shilingi 3 na senti 40 huku ile ya dizeli ikipanda kwa shilingi sita na senti 40. Bei ya mafuta taa imepanda kwa kiwango cha juu zaidi kwa shilingi 15 na senti 19. Bei hii mpya sasa inafikisha bei ya petroli jijini Nairobi kuwa shilini 182.70 huku ile ya dizeli ikifika shilingi 161.13.