Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla ndiye Mkuu mpya wa Majeshi nchini.
Jenerali Ogolla anachukua nafasi ya Jenerali Robert Kariuki Kibochi ambaye muhula wake umekamilika.
Hadi kuteuliwa kwake, Ogolla amekuwa akihudumu katika wadhifa wa Naibu Mkuu wa Majeshi.Kibochi anastaafu katika jeshi baada ya kuhudumu kwa miaka arubaini na minne.