×
The Standard Group Plc is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services. The Standard Group is recognized as a leading multi-media house in Kenya with a key influence in matters of national and international interest.
  • Standard Group Plc HQ Office,
  • The Standard Group Center,Mombasa Road.
  • P.O Box 30080-00100,Nairobi, Kenya.
  • Telephone number: 0203222111, 0719012111
  • Email: [email protected]
Premium

Je, Vladimir Putin atakamatwa?

News

Kitendawili kinazidi kuuzingria uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC wa kutoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladmir Putin.

Katika hati hiyo, ICC imemtuhumu Putin kuhusika katika uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha watoto kutoka Ukraine kwenda Urusi kinyume na sheria.

Inasema uhalifu huo ulifanyika nchini Ukraine kuanzia tarehe 24 Februari 2022 - wakati Urusi ilipoanzisha uvamizi wake kamili huku Ukraine, ikisema ina sababu za kuridhisha kuamini kuwa alifanya vitendo hivyo moja kwa moja, pamoja na kufanya kazi na wengine.

Licha ya kibali hicho huenda Putin akakosa kukamatwa jinsi ICC ilivyoagizwa. Kwanza ifahamike kwamba ICC haina mamlaka ya kuwakamata washukiwa, na inaweza tu kutumia mamlaka ndani ya nchi ambazo zimesaini makubaliano yaliyounda mahakama hiyo.

Pili Urusi si mwanachama wa makubaliano hayo - kwa hivyo hakuna uwezekano wa kiongozi huyo kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC. Na iwapo labda ungekuwapo, pia ungekuwa mchache mno kwa kuwa ndiye Rais aliye mamlakani, hivyo hawezi kuitumia mamlaka dhidi yake yeye mwenyewe.

Hata hivyo kibali cha kukamatwa kwa Putin kinaweza tu kumwathiri kwa njia nyinginezo , kama vile kutoweza kusafiri.

Tayari Rais wa Marekani Joe Biden amepongeza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC uliotoa hati ya kukamatwa Putin. Japo Marekani haiiitambui pia mahakama ya The Hague Biden anasema uamuzi huo ni wa ishara kubwa kwamba sharti haki za binadamu ziheshimiwe.

Hayo yanajiri wakati ambapo Kiongozi wa Mashtaka katika ICC Kharim Khan amesema upo uwezekano mkubwa kwamba, Rais atakamatwa na kushtakiwa katika mahakama hiyo.

Akitoa mfano wa marais ambao wamewahi kushtakiwa na hata kupatikana na hatia katika mahakama hiyo Khan amesema hilo linawapa imani kuwa tuhuma dhidi ya Putin pia zinaweza kufuata mkondo uo huo.

Akihojiwa na Runina ya CNN Khan amesema uamuzi wa Mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa Putin ni ujumbe kwa viongozi kote duniani kuwa lazima haki za binadamu ziheshimiwe.

Related Topics


.

Trending Now

.

Popular this week