Seneta wa Kakamega mheshimiwa Cleophas Malala amekumbana na wakati mgumu baada ya kukabiliwa na Baraza la Wazee wa Wanga maarufu kwa kimombo kama (Wanga Council of Elders) wakimkana peupe na mchana kwamba siyo mmoja wa familia yao. Wakiongozwa na kinara wao, Peter Nabongo wanadai kwamba seneta Malala kamwe hafai kujumuishwa pamoja na tadi na inda za jamii ya Waluhyia wakisema kwamba hapaswi kuorodheshwa katika mipango ya ndani ya kijamii kwa kuwa yeye ni wa kutoka kwa jami ya Luo.
Wanasema kulelewa kwake Kakamega hakuwezi kumfanya afure kichwa kiasi cha kujidai kuwa ni mmoja wao kikamilifu. Kwao ni kiongozi wa siasa kama mwakilishi wa bunge la seneti lakini hana nafasi ya kushirikishwa kikamilifu kijamii. Nabongo alimtaka Cleophas kujitenga na maswala yanayo husiana na jamii ya Luhya maana kwamba babake Malala alikuwa mgeni wa jamii hiyo wakati alipokelewa na kupewa hifadhi kama mgeni wa kwenda kabla ya kupata mke (mamake Malala) na kuanza kujenga famila na kusahau kurejea kwao Nyanza.