Waumini wadai Mungu wao Jehova Wanyonyi yuhai, atarejea hivi punde

Jehovah Wanyonyi.

Kwingineko ni kwamba waumini wa dhehebu la linalotambulikana  ulimwenguni kote maarufu kama Jehova Wanyonyi ambao wanapatikana  katika Kaunti ya Bungoma, magharibi mwa Kenya, wamewapa waumini wao tumaini baada ya nabii kujitokeza wazi na kudai kwamba Mungu wao ambaye ni Jehova Wanyonyi hakuaga dunia bali alikuwa kwenye ziara za kiungu na kwamba amesema naye, na kumhakikishia kwamba yu hai na atarejea muda si mrefu.

Nabii huyo ambae anadai kuwa mtumwa wa mungu wao alikuja duniani kwa ajili ya kuleta nafuu kwa waumini wanaoaminika kuwa na imani ndogo katika dhehebu hilo.

Yasemekana kwamba nabii huyo ambaye ni wa kike alitokea katika bahari moja iliyoko maeneo ya Lodwar na kwamba yeye hana jamii humu duniani bali ni mteule wa mungu ambae ni JEHOVA WANYONYI.

Haya yanajiri miaka michache tu baada ya kupata tarifa kwamba aliye kuwa mungu wa waumini hao, Wanyonyi maarufu kama Jehova aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Jehova mwenye umri wa makamo aliaga dunia kisha akazikwa kwake nyumbani katika kijiji cha Seregei kaunti ya Bungoma.

Furaha ilitanda katika kijiji hicho baada ya kupokea taarifa hizo, kwani jamii ya mungu ilikuwa na imani hiyo kwamba siku moja atarudi. Alisubiriwa sana na jamii yake ambayo ni jumla ya watu mia tatu kwani alikuwa na wake sabini.

Related Topics

Jehova Wanyonyi