Wahenga walisema usipoziba ufa, utajenga ukuta. Ufa uliojitokeza rais Pierre Nkurunziza aliposema atawania awamu ya tatu Burundi, huenda ukaporomosha misingi ya taifa hilo la Afrika kati. Hali ya pata shika nchini Burundi kwa sababu za kisiasa na kikabila zinadhoofisha uthabiti wa taifa zima.
Upatanishi lazima usisitizwe Burundi kati ya wafuasi wa serekali kwa upande mmoja na wale wa upinzani kwa upande mwingine. Ingawa upinzani unanung’unika kwamba swali nyeti ni kuwania kwa bwana Nkurunzunza kwa awamu ya tatu, ukweli wa maneno ni kwamba hata rais asipokuwepo kwenye uchaguzi huyo, hali ya wafuasi wa serekali kutisha wale wa upinzani hauwezi kusababisha uchaguzi huru.