Faida ya kiroho, kijamii na kimaadili katika Ramadhani

Waumini wa kiislamu waswali wakiadhimisha Ramadhani. [Picha: Pambazuko]

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha neema zote kubwa na ndogo.Asalam aleikum warahmatullahi taala wabarakatu.Saum Kareem..saum maqbul! Tukiwa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan hatuna budi kutowa shukurani zetu kwa Allah Jallah Jallallu kutuwezesha kuona siku ya leo. Ni wengi walioazimia kuwa katika funga hii ya saumu iliyo na faida sufufu lakini hawakuweza kwani wameenda mbele ya haki.

Mimi na wewe tuna bahati kuwa twapumuwa hewa ya Allah Azzah Wajallah kupata fursa hii adimu kuweza kuvuna mengi yaliyo katika mwezi huu unaokuja mara moja kwa mwaka. Funga ama saumu hii ya mwezi wa Ramadhani imezungukwa na neema za kila aina. Neema hizi ziko katika nukta za kijamii, kiroho, kiuchumi na kimaadili na pia kiafya.

Kuzipata neema hizi si kususia kula tu bali ni kutekeleza mema alotuamrisha Allah (SWT) hususan ibada na kuwa wachaji Mungu. Tunaelewa ile aya maarufu inayodhihiri saumu ya Ramadhan.Katika sura ya pili yaani Baqara aya ya 183 Allah (SWT) asema: “Mumeamrishwa kufunga sambamba na wale walofunga kabla yenu ili muwe wachaji Mungu” (Baqara 2: 183). Kimsingi hapa ni kuwa madhumuni makuu ya kufunga Ramadhani ni tuwe wachaji Mungu.

Uchaji Mungu huu ni kujiepusha na mabaya na kufanya mema. Kiroho, tunaona kuwa anayefunga huwa amefaulu katika maisha yajayo baada ya haya mafupi ya duniani. Twambiwa kuwa anayefunga huwa anakubaliwa dua au maombi yake haraka na Allah(SWT) kuliko yule kobe mla mtana. Kufunga kwaonyesha utwifu mkubwa kwa mola wako kwani utakuwa unakubali yale uloamrishiwa kama aya tangulizi ilivyoeleza. Mwili wa anayefunga husa?shwa na kuwa sa?  kabisa kama pamba ama mwana mchanga alozaliwa leo.

Usa? huu wa mwili ni pamoja na kuondolewa roho chafu, roho ya ibilisi, roho mbaya ya tamaa na legevu, roho ya kufata maasi , roho ya kibri na kadhalika. Twaelezwa kuwa wakati huu wa funga ya Ramadhani hakuna mashetwani kwani Allah (SWT) amewafunga chini ya bahari ili wasiharibu funga yetu. Hatahivyo kufungwa huku kwa mashetani si tiba kamilifu ikiwa nafsi yako inakutawala.

Nafsi ya mtu hushinda shetani. Funga kwa muktadha huu humaliza nafsi kwa kuipa njaa kwa kufunga. Hatahivyo sharti tuwe na azma ya kuishinda nafsi hii. Kuna wale wanaofunga tu bila kufanya ibada. Utafungaje tu kwa kususia chapati na borowa zito huku huendi msikitini kuswali? Utafunga vipi kwa kukata maini mkarango na chai nzito ya iliki na tangawizi ikiwa wewe hudiriki msikitini kusikia darsa za dini?

Kuna faida gani kuacha biriani ya kuku na sharbati ikiwa wewe husomi Quran ukijuwa ilishuka mwezi huu wa Ramadhani? Mbali na kuitufunza kuzuia nafsi zetu kufanya maovu saumu hii inatufunza kuzidisha ibadah ili tuwe karibu sana na Allah Azzah Wajallah. Kimaadili funga hii inatuendeleza kuwa watu wenye tabia nzuri badala ya kuwa wahuni wasiojali.

Inatuzuia kuwa na tamaa za kimwili kwani hata akipita mrembo kamwe humuoni hata akikuonyesha vituko vya kurembuwa. Inatufunza kuwa wakweli na waadilifu huku ikikufunza kuwa na subra. Unapofunga huwa umetulia na  hata ukiona nofu la kuku hujali. Kijamii, funga inaunganisha watu wote katika ibada moja bila kujali tajiri au masikini. Wenye nacho huwa sawa na wasonacho.

 Matajiri wapendao kula kama ndege hufahamu katika mwezi huu maana ya kukaa njaa kwani wao pia hufunga. Inatufunza kuwa na imani kwa wenzetu wasonacho kwani wanaowasaidia hupata thawabu.Ni mwezi huu ambao wengi hutowa vyakula kwa wingi. Kwa ajili hii funga hujenga undugu na utangamano wa waumini kwani watu huwa wamoja kwa tendo nyeti la ibada.

Inatufundisha umuhimu wa kugawanya vyakula, kusaidiana kuwa na huruma jambo ambalo linamaliza ula? , ubinafsi na ubahili. Kufunga huku kunapunguza majivuno na kibri kwani wale matajiri ambao hujivuna kuwa hawalali njaa hulazimika kukaa njaa na kibri huyeyuka. Kiafya funga ya Ramadhani huboresha miili yetu pakubwa.

Wataalamu wa matibabu wanedhihirisha kuwa wanaofunga ni watu wa afya. Wakati wa kufunga mwili wetu huweza kupumzika kutokana na malaji na hivyo kufanya mwili kujijenga kwa kupumzika. Kufunga hufanya manyama kupunguwa na kumaliza ule unene usio na maana (obecity) kwani ni maradhi.

Kwa kufunga waumini hujitayarisha kuwa ngangari ikiwa kuna njaa kwani watahimili kuliko wale wanaokula kama ndege. Yarabi twamuomba Allah (SWT) atukubaliye funga yetu na kuweza kuvuna mema na neema iliyo ndani ya mwezi huu mtukufu.Amina. Wabillahi taw? q. Jazakallahu kheir. Ahlan wasahlan wamarhabaa.

Business
Tea factory directors face opposition in elections
Financial Standard
Premium Gikomba gold rush: Banks scramble for a slice of Nairobi's street hustle
By XN Iraki 2 hrs ago
Financial Standard
Premium Yes, prices are falling but it might be too early to celebrate
Financial Standard
Premium Inside Sh5b NOC-Rubis deal to revamp cash-strapped oil marketer