Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Aden Duale ameponea shoka la Chama cha Jubilee wakati wa kikao cha wabunge kilichoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta mapema leo hii.
Chama cha Jubilee kimefanya mabadiliko katika uongozi wake bungeni ambapo Kiranja wa Wengi Benjamini Washiali na Naibu wake Cecily Mbarie wamevuliwa rasmi madaraka.