Hospitali ya Kenyatta yapinga kumtelekeza Prof Walibora

Wakenya hasa katika mitandao ya Jamii wamegadhabishwa na hatua ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, KNH ,kukana kwamba ilimletelekeza kwa muda wa saa kumi na nane mwandishi mahiri, mwanahabari na mhakiki wa lugha ya Kiswahili Profesa Ken Wabora Waliuala na hivyo basi kusababisha kifo chake.

Baadhi ya hisia zilizotolewa katika mitandao ya kijamii ni kuwa hospitali hiyo inajitetea baada ya kulaumiwa kwa kifo cha Walibora.

Afisa Mkuu Mtendaji wa KNH Daktari Evanson Kamuri  amesema kwamba taasisi hiyo ilifanya iwezalo kumshughulikia Profesa Walibora alipofikishwa  kutibiwa baada ya kugongwa na basi kwenye Barabara ya Landhies Aprili 10.

Dakta Kamuri amesema kuwa Walibora alipelekwa katika chumba cha dharura punde alipofikishwa humo na kuhudumiwa kabla ya kufariki dunia kutokana na majeraha mabaya aliyokuwa nayo.

Kamuri amesema kuwa Walibora alikuwa na majeraha kichwani huku akishindwa kupumua na kwamba madaktari wakati wote walimshughulikia kabla ya kufariki dunia na kupuuza uvumi kwamba alitekelezwa.

Alikuwa akijibu maswali wakati wa kikao na Kamati ya Seneti ya Afya inayoongozwa na Seneta wa Trans Nzoia Michael Mbito alipotakiwa kutoa mwanga zaidi kuhusu suala hilo.

Wakenya mitandaoni waliendeleza shutma  dhidi ya KHN kwa madai ya kumtekeleza Walibora kwa saa kumi na nane alipofikishwa humu wakisema kwamba madakatari wa hospitalii hiyo walichangia kifo cha mwandishi huyo. Wakenya aidha walionesha ghadhabu kwamba KNH imekuwa ikiwatenga wangonjwa wengine na kuwahudumia wa virusi vya korona pekee.

Walibora alitoweka na kisha baadaye mwili wake kupatikana KNH akidaiwa aligongwa na basi alipokuwa akiwatoroka watu fulani waliokuwa wakimfukuza. Uchunguzi unaendelea kuhusu kifo chake baada ya Mwanapotholijia Mkuu wa Serikali Dakta Johsen Oduori kubaini kwamba alikuwa na jeraha la kisu kwenye viganja vyake.