KNUT: Sossion atajua maharagwe ni mboga

Wilson Sossion.

Muungano wa waalimu nchini KNUT umejulikana kwa mda mrefu kama muungano wa kutetea msalahi ya wanachama wake kwa ari na nguvu ya kipekee kutokana na wingi wa wananchama wake ambao ni walimu wa shule za msingi na baadhi ya wale wa shule za upili.

Maafisa wake wakuu ambao wamekuwa wakichaguliwa ndani ya fani ya ukufunzi, ama waliokuwa walimu kwa wakati mmoja, wameonakana kunoa makali kila kuchao kukabiliana na muajiri wa waalimu wa shule za umma ambayo ni Tume ya kuajiri Waalimu TSC.

Tangu jadi makatibu wa KNUT wameonakana kukabiliana na serikali ana kwa ana bila ya uoga wowote licha ya Serikali kutumia mbinu ya kufedhehesha kama vile kuwatia nguvuni kwa kukaidi amri ya mahakama au kunyimwa ruhusa ya kukongamana.

Ujasiri ambao kwa wakati mmoja umeonekana kulemaza shughuli za elimu nchini kwa mfano mwaka 2013 punde tu baada ya serikali ya Jubilee kutwaa uongozi, Chama cha KNUT kiliitisha mgomo uliomlazimu waziri wa Elimu kwa wakati huo Profesa Jacob Kaimenyi kufunga Shule zote za umma kwa zaidi ya siku 100.

Hata hivyo muungano wa walimu nchini KNUT umekabiliwa na msukosuko wa uongozi kutokana na tofauti za kimsimamo kati ya mweyekiti na katibu mkuu kuhusu kutekelezwa kwa shughuli za kuwapandisha vyeo walimu, kuongezwa mishahara walimu waliofuzu shahada ya digri na utekelezwaji wa mtaala mpya wa elimu unaozingatia sana masomo anayofanya vizuri mwanafunzi - maarufu CBC.

Msukosuko huo ulioshuhudiwa ndani ya muungano wa KNUT umeonekana kutumiwa na wapinzani wa muungano huo kumtimua katibu anayeondoka Wilson sosion kwa kutumia kundi pinzani na fedha zinazo wasilishwa kutoka kwa mishahara ya wanachama.

Wapinzani wa KNUT walizua msukosuko na tofauti kuhusiana na Mtaala mpya ambapo katibu huyo mkuu alitofautiana na jinsi serikali kupitia wizara ya elimu ilipanga kuutekeleza kwa haraka.

 Kadri siku ziliposonga mawimbi yakaonekana kumzidi Muheshimiwa Sossion aliyeonekana kushindwa kulidhibiti usukani gari la KNUT na kusababisha kujiondoa kwa zaidi ya waalimu 18,000 kwa mda usiozidi wiki mbili.

Kuchelewa kuwasilishwa kwa fedha zinazokatwa walimu kama ada ya chama kumeyafanya mambo kuwa magumu zaidi katika Afi si kuu za muungano wa KNUT hata wakati mmoja Bwana Sossion kutishia kusitisha shughuli katika makao makuu ya chama Jijini Nairobi.

Juhudi za Sossion kuandaa mkutano wa Baraza kuu la chama hicho Alhamisi iliyopita, zilitatizwa na wapinzani waliokuwa wamepokea fununu za kuwepo kwa mkutano huo na kutwaa ilani ya mahakama kuzuia kufanyika kwa mkutano.

Aidha kundi pinzani lilifahamu kwamba Bwana Sossion angetumia mapendekezo ya mkutano wa Agosti 7 aliouongozwa yeye binafsi kwa mujibu wa kifungu cha 9 Ibara ya pili mstari wa tatu katika katiba ya muungano huo wa KNUT.

Hata hivyo kundi pinzani liliitisha mkutano Agosti 27 na wanachama wa baraza kuu la chama hicho waliitisha mkutano kuzungumzia ajenda tofauti na ile iliyokusudiwa kuzungumziwa Agosti 29 hii ikiwa ni mkutano uliyoitishwa na bwana Sossion.

Mipango haya yote yaliwekwa siri na kundi la pili liloonekana kumtumia Naibu wa katibu mkuu kufanikisha mipango ya kumng’atua mamlakani Bwana Sossion, Naibu wa katibu mkuu anaruhusiwa kikatiba kuitisha mkutano wa Baraza kuu pale ambapo Katibu mkuu hayupo.

“Kwa mda huo wote tumekuwa tukikutana na tunamfahamu yeye vizuri, Sossion ni mtu anayebainika kwa urahisi sana. Tulijua angeahirisha mkutano aliyokuwa ameuitisha ndiposa tumeamua kutumia mbinu ya pili,’’ alisema mmoja wa wakuu wa chama hicho kutoka kundi pinzani.

Kundi hilo la pili katika muungano wa KNUT limekuwa na viongozi wakuu miongoni mwao Mwenyekiti Wycli­ e Omucheyi, Mweka Hazina John Matiang’i Naibu wa Katibu Mkuu Hesborn Otieno Agolla miongoni mwa wengine.

Dhoruba lilizidi katika muungano huo wenye nguvu zaidi nchini, siku ya ijumaa baada ya Bwana Wycli­ Omucheyi na Bwana Hesbon Ogolla aliyeteuliwa katibu mkuu kukariri kwamba hatua yao haija hujumu kivyovyote ilani ya mahakama iliyozuia kufanyika mkutano wa baraza kuu.

‘Mkutano wetu haukutegemea mjadala wa tarehe 7 Agosti, hiyo ndio iliyozuiliwa na Mahakama, Mkutano wetu uliiegemea maombi yaliyo wasilishwa Agosti 27, na tuliafi kia matakwa yote ya katiba yetu,’’ alisema Bwana Omucheyi.

Aidha kwenye taarifa ya awali kwa wanahabari kundi hasimu lilitangaza kwamba Sossion atasalia kuwa nje ya Afisi yake hadi mwezi Disemba mwaka huu pale ambapo kungeandaliwa mkutano wa wajumbe wa kitaifa kupiga kura na kuyapitisha mabadiliko yaliyofanyiwa viongozi wa muungano huo.

Aghalabu makali yaliyowabana wanachama kutokana na uhusiano uliombovu kati ya Sossion na maafi sa wakuu serikali imebadili kasi ya kuandaliwa kwa mabadiliko kwenye muungano wa KNUT kupisha viongozi wapya.

“Wanachama wetu wanateseka kwa sababu hatujakuwa na uhusiano mwema kati yetu na wakuu serikalini na tume ya Kuajiri Walimu-TSC, amemtukana waziri wa Elimu Bwana Magoha, akawavuruga wakuu kwenye tume ya TSC na kukabiliana na hata Afi si ya Rais,’’ alisema Bwana Agolla.

Mrengo huu pia unalalamika kuhusu hatua ya sossion kushughulikia matakwa yake badala ya kuongoza kikosi kizima cha KNUT kupigania haki za walimu.

Mawimbi yalionekana kuwa makali zaidi kwa Sossion baada ya msajili mkuu wa vyama vya kuwatetea wafanyakazi Bi. E N Gicheha kumuandikia bwana Sossion Barua ya kumjulisha kuhusu kubadilishwa kwa maafi sa wakuu wa KNUT.

Sossion kwa upande wake alimjibu akitishia kumchukulia hatua za kisheria kwa kufanyia fedheha ilani ya mahakama.

Kupitia kwa wakili wake bwana J A Guserwa alimtaka Bii Gicheha kuondoa mabadiko hayo la sivyo amchukulie hatua za kisheria.

Ikiwa Bwana Sossion atakosa kujinasua kwenye mtego huu wa kubanduliwa kwenye uongozi wa KNUT, hofu inawaingia viongozi wa vyama vingine vya wafanyakazi wanaoonekana kutatiza mipango ya Serikali wakiogopa mizozo chamani inaweza kutumiwa na vibaraka wa serikali kuwatimua uongozini.