Mwanaume akamatwa baada ya kummwagilia mwenzake asidi

Maafisa wa polisi wa Machakos mjini wamemkamata mwanaume mmoja ambaye amemjeruhi mwenzake wa umri wa makamo kwa kummwagilia asidi kwenye sehemu zake za siri kufuatia tofauti baina yao walipokuwa wakivinjari, katika soko la Kathome lililo kijiji cha Kalama, Kaunti ya Machakos.

Mwanamume huyo anaendelea kutibiwa katika hospitali ya Machakos level 5 anaeleza alikuwa katika baa moja akiwa na wenzake na wakati wa kuondoka ndipo mvutano ukaanza  kisha mshukiwa akamwangusha na akammwagilia asidi hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Machakos mjini Joseph Tenai amesema mshukiwa  anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Machakos huku uchunguzi ukiendelea.

Register to advertise your products & services on our classifieds website Digger.co.ke and enjoy one month subscription free of charge and 3 free ads on the Standard newspaper.

machakos county