Radio Maisha yaadhimisha miaka 9

Na Rosa Agutu,

NAIROBI, KENYA, Kituo cha Redio Maisha leo hii kinaadhimisha miaka tisa tangu kuzinduliwa 2010. 

Idhaa hii imeendelea kuimarika na kuteka anga na nyoyo za wengi ndani na nje ya nchi kwa vipindi bomba na habari za hivi punde na za kuaminika.

Hafla ya kusherehekea miaka 9 tangu kuanzishwa kwa idhaa hii tarehe 24 Mei 2010, imefanyika katika makao makuu ya Shirika la Standard Group mkabala na Barabara ya Mombasa hapa Nairobi na kuhudhuriwa na Bodi-simamizi na wakuu wa shirika hili.

SEE ALSO :Pensioners turn to Kenya's DCI in new bid to recover Sh1.2b assets

Mkuu wa Radio Maisha, Tom Japanni amewapongeza wasikilizaji, watangazaji na uongozi wa Standard Group kwa ujumla kwa kuchangia katika mafanikio yote haya.

Kilele cha maadhimisho hayo ya miaka tisa kitakuwa wakati wa Choma na Ngoma tarehe 31 mwezi huu katika ukumbi wa KICC.

Kumbuka Redio Maisha ndicho kituo nambari moja kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini CA, kwa kuwa chaguo la wengi.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.