Ombi la Kidero latupiliwa mbali na mahakama

Mahakama jijini Nairobi imetupilia mbali ombi la aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Nairobi, Evans Kidero kutaka kesi zinazomkabili kutojumuishwa wakati wa kusikilizwa.

Jaji Douglas Ogot ametupilia mbali ombi hilo akisema upande wa mshtakiwa haujatoa sababu mwafaka kuishawishi mahakama kukubali ombi lenyewe.

Kwenye kesi hiyo, Kidero na waliokuwa wafanyakazi wakati alipokuwa gavana, wameshtakiwa kwa utumiaji mbaya wa ofisi, hali iliyosababisha kufujwa kwa fedha, vilevile wizi wa fedha hali iliyotishia kuzorota kwa uchumi jijini Nairobi.

Watakaoshtakiwa pamoja ni Kidero ni; Aliyekuwa Karani wa Kaunti Lilian Ndegwa, Jimmy Mutuku Kiamba, Gregory Mwakanongo,  Stephen Ogago Osiro,  Luke Mugo na Maurice Ochieng Okere.

Wakati wa kuwasilishwa kwa ombi lenyewe, Kidero amemshtumu Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Noordin Hajji kwa kumfungulia misururu ya mashtaka ya ufisadi kwa lengo la kumpaka tope.

 

Related Topics