Moto wawaka katika Jumba la 2oth Century jijini Nairobi

Taharuki imetanda jijini Nairobi, baada ya Moto mkubwa kutokea katika jengo la 20th Century kwenye Barabara ya Mama Ngina. Moto huo ulianza mwendo wa saa saba mchana leo kwenye vyumba vya juu vya ghorofa hiyo na chanzo chake hakijabainika.
Wazima-moto tayari wamefika kuukabili moto huo ambao umezua hofu na kusitisha shughuli kwenye jengo hilo na maeneo ya karibu.

Jengo hilo lenye shughuli chungu zima, ni makao ya IMAX Cinema Theatre, Mkahawa wa Dancing Spoon na biashara mbalimbali ambazo zimeathirika. Tutakupasha mengi wakati wa habari zetu zijazo.

We are undertaking a survey to help us improve our content for you. This will only take 1 minute of your time, please give us your feedback by clicking HERE. All responses will be confidential.