Wakenya waendelea kumpongeza Mwalimu aliyetuzwa shilingi milioni 100

Rais Uhuru Kenyatta amewaongoza wakenya katika kumpongeza mwalimu Peter Tabichi Mokaya mwenye umri wa miaka 36 kwa kushinda tuzo ya mwalimu bora duniani tuzo inayofadhiliwa na Wakfu wa Varkey.

Tabichi ambaye ni mwalimu wa Kemia na Hisabati vilevile mtawa wa Kiume katika Kanisa Katoliki amejishindia shilingi milioni 100kufuatia juhudi zake  za kutumia raslimali finyu ukiwamo asilimia 80 ya mshahara wake ili kuwanufaisha wanafunzi katika Shule ya Keriko kwenye Kaunti ya Nakuru vilevile wakazi.

Peter Tabichi Mokaya ametangazwa mshindi katika hafla ilioyofanyika katika mji wa Dubai.

 

Rais Kenyatta amemtaja kuwa mfano wa kuigwa baada ya kuiletea Kenya na Afrika kwa jumla sifa baada ya kuwa pekee wa asili ya kiafrika kuteuliwa na hatimaye kushinda.

Kufuatia juhudi zake, wanafunzi wawili miongoni mwa wanafunzi wake watashiriki mashidnano wa kisayansi Marekani baada ya kuteuliwa miongoni mwa wanafguzni 1800 bora duniani. Tabichi ametaja uamuz wake wa kufuata mkondo wa utawa wa kiume katika kanisa katoliki kutokana na nia yake ya kujituma kwa jamii. Tuzi yake ya shilingi milioni 100 itatolewa kwa awamu kwa miaka 10 ijayo na anatarajiwa kuitumia kuendeleza miradi yake katika jamii.

Mwalimu Mkenya Maina Kioko vilevile alifika awamu ya 50 bora kabla ya idadi kupunguzwa hadi watu 10.

Related Topics