Madaktari 250 kugoma Kisumu

Madaktari wanaohudumu katika Kaunti ya Kisumu sasa wametisha kugoma kuanzia saa sita leo usiku  baada ya serikali ya kaunti hiyo kupuuza  notisi yao ya mgomo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari KMPDU tawi la Nyanza, Kevin Osuri, serikali ya kaunti hiyo imekataa kuwasikiliza wanapolalamikia kutotekelezwa kwa baadhi ya vipengele vya makubaliano ya kurejea kazini ya mwaka 2017.

Miongoni mwa masuala hayo ni ulipaji mishahara  ambapo baadhi wanadai hawajalipwa kwa takribana miezi mitatu. Vilevile wanataka waruhusiwe kuchukua likizo za masomo kadhalika kuhakikisha matozo ya mishahara yao inawasilishwa kwa idara zinazohusika.

 

Madaktari hao zaidi ya 250 wamewataka wakazi kujitayarisha  kukosa huduma zao wakilalamika kwamba licha ya kuwa Kaunti ya Kisumu ni miongoni mwa zinazofanyiwa majaribio katika mpango wa Afya Bora kwa Wote, hali ni mbaya.