William Ruto azitaja kuwa ufisadi, siasa zinazoendelezwa.

Naibu wa Rais, William Ruto amezitaja kuwa  ufisadi, siasa zinazoendelezwa kwa misingi ya kukabili jinamizi hili. Akihutubu wakati wa halfa moja kwenye Kaunti ya Mombasa, Ruto amesema licha ya serikali kuwekeza kwa idara zilizojukumiwa kukabili ufisadi, kuna watu walio na njama fiche ambao wanalenga kuzitumia idara hizo kwa manufaa binafsi.

Siku chache zilizopita Ruto alimshtumu Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi, DCI George Kinoti kwa madai ya kutumiwa kisiasa katika njama ya kutatiza miradi ya maendeleo ya serikali kwa kisingizio cha kukabili ufisadi japo Kinoti amesisitiza kuwa ofisi yake haitatishwa na  yeyote katika kutekeleza majukumu yake.

Kwa mara nyingine Ruto amejitetea kwa kuzungumzia utata unaozingira ujenzi wa mabwawa ya Aror na Kimwarer akisema akiwa Naibu wa Rais, ni jukumu lake kufahamu kuhusu miradi inayoendelea.

Ikumbukwe Kinara wa Chama cha ODM, Raila Odinga ni miongoni mwa waliomshtumu hadharani kwa kuzungumzia suala la ujenzi wa mabwawa hayo akisema huenda ana njama fiche na kumtaka kuziruhusu idara za uchunguzi kukamilisha uchunguzi wake fedha zinazodaiwa kupotea kupitia miradi hiyo

Related Topics

William Ruto