Viwango vya riba kubadilika baada ya miezi 12

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Wakenya walio na mikopo katika benki sasa wana afueni ya miezi 12 kabla ya kuanza kutekelezwa kwa agizo la mahakama lililotaja sheria ya udhibiti wa viwango vya riba kuwa kinyume na sheria.

Uamuzi huo ulifuatia kesi iliyowasilishwa na Mkenya mmoja kwa jina Bonface Oduor kupinga sheria hiyo iliyoweka kiwango cha riba kuwa  kisipite asilimia 4 ya kile kinachowekwa na Benki ya Kuu Kenya.

Kufuatia sheria hiyo wakenya wamekuwa wakilipa riba ya katyi ya silimi 13 na 14.5 tofauti na awali riba ilifikia hata asimilia 20.

Kwasasa, bunge lina miezi 12 kuwazia sheria hiyo iwapo hakutakuwa na rufaa kufuatia uamuzi huo.

Related Topics

Benki