Ukeketaji wavunja ndoa katika jamii

Picha kwa hisani ya mtandao

Ukeketaji wavunja ndoa katika Kaunti ya Taita Taveta,huku kaunti hiyo ikiongoza kwa asilimia 61.3 ya visa vya watoto wadogo wa chini ya miaka tano(5) kukeketwa.

Takwimu kutoka Kwa wizara ya afya humu nchini zinayonyesha kuwa asilimia 22 .3 ya wanawake kati ya umri wa miaka kumi na (15 ) hadi arobaini na (49 ) wamekeketwa katika Kaunti ya Taita Taveta.

Hii imechangiwa na baadhi   ya wazazi kuwakeketa watoto wao pindi tu wanapozaliwa iki kuepuka kunaswa na mkono wa sheria.

Baadhi ya waathiriwa sasa wanakabiliwa na masaibu,  ndoa zao zikiathirika pakubwa kutokana na hali hiyo walioitaja kuchangia kwa idadi ndogo ya watu katika kaunti hiyo ambayo kulingana na shirika la idadi ya watu  nchini Kaunti ya Taita Taveta  iko na takriban wakaazi 284657.

Eneo la Taveta takriban kilomita 110 kutoka Voi ndilo lililoathirika zaidi,hali ambayo imewalazimu kina mama miongoni mwao Agnes Nangondo ambaye  ni Mfawidhi(MC)wa  kipekee wa kike kulivulia njuga suala la ukekeketaji.

Kwa kawaida Agnes  huanza siku yake asubuhi na mapema na hapa tunakutana naye katika pilkapilka zake za kila siku.

Kikao cha kwanza cha Agnes kilianzia katika zahanati ya Malukiloriti ambayo ilijengwa mwaka wa 2016 kabla ya kufungwa na Kaunti hiyo Kwa misingi kuwa ilikuwa katika mazingira duni.

Kufungwa kwa zahanati hiyo  kukawa ni afueni kwa Agnes ambaye huitumia kufanywa vikao vya kuwakusanya kina mama kuwahamasisha dhidi ya athari za ukeketaji Kwa wasichana.

"Habari za asubuhi,asanteni Sana Kwa kuja kina mama,tulikuwa tunawasubiri ,tuanze mafundisho yetu ya Leo"alianza Kwa kuwaamkua."nafurahi sana hamkukutana na wakeketaji....."

Agnes anasema wakati wa likizo ndio huandaa vikao vingi, ikizingatiwa kuwa wasichana wengi hupelekwa jandoni wakati huo kwa ajili ya ukeketaji.

"Wakati huo tunafanya baraza baada ya wiki mbili au tatu kuhamasisha wazazi na saa zingine pia tunakaa na watoto na tunawaeleza athari ya kukeketwa".alisema Agnes

Lakini je ni nini haswa kilichomshawishi kuanzisha kampeni hiyo?

Turudi nyuma kidogo

Agnes ambaye ni mzaliwa wa Taveta ni mwathiriwa wa ukeketaji hali ambayo anasema imeathiri pakubwa ndoa yake.

"Kilichoniifanya Mimi zaidi kuingilia masuala dhidi  ya ukeketaji no kwasababu mimi ni mojawapo niliyekeketwa.nilivyo keketwa nilipolalamika hizi sherehe za kinyumbani"alisumulia Agnes.

Anasema Maisha yake yalikuwa sawa hadi pale alipopata mchumba nakuoelewa.Kilichofuatia katika Maisha  yake ilikuwa ni laiti ningalijua.

"Nilivyoolewa kuna jambo ambalo nililiona katika ndoa yangu,kwa sababu mume wangu aliniacha na akatafuta  mwanamke mwingine nje.sababu kuu ikiwa ni kuwa alipoteza sehemu za hisia"alielezea Agnes.

Malalamishi ambayo Agnes anasema yalimskuma kuanzusha kampeni dhidi ya  ukekeketaji  wa watoto  wakike,baada  ya kubaini kuwa webzake aliokuwa nao pia walikuwa wanapitia Hali sawia na yake.

Agnes ambaye amekuwa mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu kwa miaka kumi sasa,anasema walianza na kikundi kimoja kilichozaa wenzake waliounga mkono juhudi hizo.

"Kuna vikundi tofauti tofauti,kuna wengi wako mahoho,Mata na bomeni.tumekuwa tunatembelea vikundi haswa haswa sehemu ambapo ukeketaji unaendelezwa"alisema Agnes

Eneo la mboghoni  ndio kitovu cha shughuli hiyo,baadhi ya wasichana ambao hawajapitia ukeketaji  wakipitia unyanyapaa.

"Suna" ndilo jina wanalotumia kwa wale waliopitia ukeketaji licha ya athari zinazotokana na shughuli hiyo ikiwemo kuvunjika Kwa ndoa na vifo kutokana na kuvuja  damu  Kwa msichana  anaopikeketwa.

"Usipotairiwa au kukuketwa baada ya kufikisha umri fulani ukienda mahali ambapo  kuna wenzako ,watakucheka." Aliongeza kusema Agnes.

Swala la ukeketaji wa wasichana katika Kaunti ya Taita Taveta limewakosesha usingizi wakereketwa wa kutetea haki za kibinadamu, Agnes akiapa kuendelea na harakati hizo hadi pale ukeketaji utakapokomeshwa.

Kuwanasua wasichana watatu kutoka jamii  ya kimaasai ikiwa ndio baadhi tu ya Matunda yanayomshinikiza  Agnes na kampeni hiyo ambayo imewaokoa wasichana kadhaa Taveta.

Licha ya kutokamilika  kwa kesi dhidi ya wahusika wanaoendeleza shughuli hiyo,Agnes anasema hajakata tamaa na kuonesha matumaini kuwa siku moja haki itapatikana.

Kikuu kabisa Kwa Agnes no baada ya kukutana na mama masumbua masambo ,bibi wa  takriban miaka 70 ambaye alikuwa ni mkeketaji kabla ya kuachana na shughuli hiyo baada ya hamasa.

"Sijui nimefanya shughuli hii kwa miaka ngapi Kwanza nimeacha kwasababu serikali imekataa,pili watoto wake wote walikataa."alisema Bibi Masumbuo.

Kulingana na Agnes tatizo la ukeketaji litaisha  endapo jamii itakubali kuachana na sheria ya ambazo zinachangia  unyanyapaa kwa wasichana ambao hawajakeketwaTakwimu za hivi punde kutoka kwa shirika la kutetea haki za kibinadamu la haki Africa zinayonyesha kwamba  kiwango cha wasichana wanaokeketwa katika Kaunti ya Taita Taveta ni asilimia(60 %)huku asilimia( 20%)wakipoteza maisha yao kutokana na kuvuja damu.

Kaunti ya Taita Taveta ni Kati ya  maeno 17 humu nchini yanayomulikwa sana  kwa sababu ya  ukeketaji wa wasichana .