Naibu wa Rais William Ruto ametakiwa kurekodi taarifa kuhusu anachojua kufuatia sakata ya mabwawa ya Aror na Kimwarer

Na Esther Kirong'

Nairobi Kenya, Naibu wa Rais William Ruto ametakiwa kurekodi taarifa kuhusu anachojua kufuatia sakata ya mabwawa ya Aror na Kimwarer ambapo fedha takriban shilingi bilioni 21 zinadaiwa kufujwa.

Mbunge wa Tiaty, William Kamket aidha amemtaka Ruto kukoma kuzungumzia sakata hiyo kwenye mikutano ya hadhara. Akizungumza katika mtaa wa Akwichatis, Kamket amesema kauli zinazotolewa na viongozi mbalimbali kuhusu sakata ya ufujaji wa shilingi bilioni 21 zitakuwa muhimu iwapo viongozi hao watashirikiana na idara za uchunguzi. Aidha anasema serikali itahakikisha wahusika wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha amemsuta Ruto kwa kudai kwamba ni shilingi bilioni 7 ndizo zimefujwa na wala si shilingi bilioni 21 jinsi inavyodaiwa na idara ya upelelezi.

 

Related Topics

Ruto Aror