Matamshi ya Rais Kenyatta kuwaita watu fulani ''washenzi'' yaendelea kuibu hisia

Wanasiasa wa eneo la Kati ya Nchi wakiwamo wabunge wa sasa na wa zamani, waliokuwa mawaziri na viongozi wengine wa kisiasa eneo hilo siku ya Jumatano wanatarajiwa kuwahutubia wanahabari kuhusu masuala kadhaa ya uongozi.

Miongoni mwa masuala hayo ni hali ya siasa katika Chama cha Jubilee, hali ya mwafaka wa ushirikiano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga, rekodi ya maendeleo ya Uhuru, ushirikishi sawa wa kisiasa na suala la kuandaliwa kwa kura ya maamuzi.

Hayo yanajri huku Naibu wa Rais William Ruto akimtetea Rais Kenyatta kuhusu rekodi yake ya maendeleo.Kupitia mtandao wake wa Twitter, Ruto amewasuta baadhi ya wanasiasa wa Jubilee wanaodai kuwa eneo la Kati ya Nchi limetengwa kimaendeleo na kujaribu kuwadhalilisha viongozi wa chama na Rais.

Ruto amesema serikali itahakikisha hakuna eneo linatengwa kimaendeleo na kuwataka wanachama wa Jubilee kutumia njia zinazofaa kuwasilisha malalashi bila kuibua mgogoro chamani.

Anaendelea kusema nikimnukuu,  

After projects promised for decades became a reality under Jubilee many Kenyans especially Jubilee members understandably are asking us for more. This must be tempered with the reality of what we can afford. No region, community or Kenyan will be left behind now or in future,

Mwisho wa nukuu.

Kauli ya Ruto ilijiri saa chache jana baada ya sarakasi za hapa na pale kushuhudiwa siku nzima miongoni mwa viongozi wanaomshtumu Rais Kenyatta kwa madai ya kulitenga eneo la kati na hata kuwaita Washenzi wale wanaomkosoa kuhusu utendakazi wake huku wengine wakijitokeza kumtetea.

Wabunge kumi na mmoja wa eneo la Mlima Kenya wakiongozwa na Mbunge Maalum, Cecily Mbarire walifanya kikao katika majengo ya bunge kumtetea Rais wakisema tangu Jubilee ilipochukua hatamu za uongozi mwaka wa 2013, kumeshuhudiwa maendeleo kwenye kila eneo nchini hivyo, Rais hajalitenga eneo la Mlima Kenya.

Kauli sawa na hiyo ilitolewa na Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu alipokuwa akihutubu katika halfa tofauti huku akitetea rekodi ya maendeleo ya Rais.

Awali mchezo wa paka na panya ulishuhudiwa baina ya maafisa wa polisi na Mbunge wa Bahati, Kimani Ngunjiri aliyeandamana na kundi la vijana kupinga kauli ya Rais Kenyatta kwamba baadhi ya viongozi wa eneo la Mlima Kenya wanaoshinikiza maendeleo ni Washenzi. Walivalia mashati-tao yenye maandishi Mimi ni Mshenzi, Je, Wewe MwanaKenya? 

Kutokana na maandamano yao Kamanda wa Polisi kaunti ya Nakuru, Hassan Barua na OCPD Samuel Obara walimesema walijarubu kumnasa mbunge huyo japo alikwepa kupitia mlango wa nyuma wa hoteli moja huku ikiarifiwa kwamba angali anasakwa na polisi.  Kimani sawa na Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria wamemshtumu Rais kwa madai ya kulitenga eneo la Mlima Kenya kimaendeleo.  

Related Topics

Uhuru washenzi