Gavana wa Migori, Okoth Obado amejitokeza hadharani leo hii kwa mara ya kwanza kukana kuhusika katika mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno. Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi akiwa ameandamana na mkewe, wanawe wawili na maafisa wengine wa Kaunti ya Migori, Obado amesema kwamba kuhusishwa na kisa hicho kumeisababishia mahangaiko makuu familia yake.
Obado ametoa wito kwa maafisa wa usalama wanaochunguza mauaji ya Sharon kuharakisha uchunguzi ili wahusika wakuu wakabiliwe kwa mujibu wa sheria.