KESI YA BERO ZILIZOGHARIMU LAKI MOJA YAENDELEA

Na Mike Nyagwoka/Chrispen Sechere

Kwa mara nyingine maafisa watano waliokuwa wafanyakazi wa serikali ya Kaunti ya Bungoma wamefikishwa katika Mahakama ya Kakamega ambako wameshtakiwa kwa tuhuma za ufisadi kuhusu ununuaji wa bero tisa, yaani wheelbarrows mwaka wa 2014.

Shahidi kwenye kesi hiyo, Isaya Kisiangani ambaye ni mfanyakazi wa serikali hiyo katika idara ya mifugo amekuwa wakati mgumu kujibu maswali huku wakili wa washtakiwa Sylvester Madialo, akimtaka kueleza ni kwa nini aliamua kubadili taarifa yake ya awali kuwa aliishauri kamati ya zabuni ya serikali ya Bungoma kuhusu bei za vifaa hivyo. Imeilazimu mahakama kusitisha kikao cha mahojiano baada ya shahidi huyo kudai anaugua ugonjwa wa moyo.

Washtakiwa wakiwamo Juma Matsanza, Howard Lukadilu, Oscar Onyango na Jacklin Nanjala wanatuhumiwa kununua bero hizo kwa shilingi elfu 109,320 kwa kila bero, hivyo kukiuka kipengele cha 121 cha sheria za matumizi ya fedha za umma.

Related Topics