Usipoziba ufa, utajenga ukuta: Changamoto zinazoikumba taifa la Burundi

Wahenga walisema usipoziba ufa, utajenga ukuta. Ufa uliojitokeza rais Pierre Nkurunziza aliposema atawania awamu ya tatu Burundi, huenda ukaporomosha misingi ya taifa hilo la  Afrika kati. Hali ya pata shika nchini Burundi kwa sababu za kisiasa na kikabila zinadhoofisha uthabiti wa taifa zima.

Upatanishi lazima usisitizwe Burundi kati ya wafuasi wa serekali kwa upande mmoja na wale wa upinzani kwa upande mwingine. Ingawa upinzani unanung’unika kwamba swali nyeti ni kuwania kwa bwana Nkurunzunza kwa awamu ya tatu, ukweli wa maneno ni kwamba hata rais asipokuwepo kwenye uchaguzi huyo, hali ya wafuasi wa serekali kutisha wale wa upinzani hauwezi kusababisha uchaguzi huru.

Vyama vya upinzani havijapewa uhuru wa kueneza kampeini zao nje ya Bujumbura. Pia, kuna hali ya wafuasi wa serekali kutisha wanahabari, kuwaua wapinzani wa Nkurunziza na pia kuwachochea wadau wa tume huru ya uchaguzi.

Jambo jingine ni swali la wakimbizi waliotorokea nchi jirani. Wakimbizi hawa inabidi wahamasishwe kurudi Burundi hali ya utulivu utakaporejea. Kwa wakati huu, hali ya utulivu haipo.

Kwa wakati huu, ni vigumu kuwa na uchaguzi huru usio na bughdha, vitisho na udanganyifu. Ni jukumu kuu kwa wapatanishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki, viongozi wa mataifa yote ya Umoja wa Afrika (AU) na wafadhili wa Burundi kama Umoja wa Ulaya na Marekani kuhamasisha pande zote mbili kuafikiana kusuluhisha hali tete iliyopo nchini Burundi.

 

Professor David O. Monda

Dept. of Social Science

National University - California. 

Ph: +1-011-424-232-1792