You are here  » Home   » News

KMPDU wapewa wiki mbili kukamilisha mazungumzo na wanachama

By | Published Thu, January 12th 2017 at 11:32, Updated January 12th 2017 at 11:45 GMT +3

Na Mate Tongola
NAIROBI, KENYA, Viongozi wa Muungano wa Madaktari, KMPDU wamepewa kipindi cha wiki mbili kukamilisha mazungumzoo na wanachama wake kuhusu kusitishwa kwa mgomo wao la sivyo wafungwe jela kwa mwezi moja.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji, Hellen Wasilwa amesema kuwa viongozi hao walikiuka sheria kwa kukosa kufika mahakamani jinsi walivyoagizwa na hivyo kuitoiheshimu mahakama.
Tayari serikali za kaunti zimeanza kuwaandikia barua madaktari wanaogoma wakitakiwa kueleza sababu za kuhisi kwamba hawafai kuchukuliwa hatua kwa kukataa kurejea kazini.
Madaktari wa Kaunti ya Nairobi, wana siku saba kufanya hivyo kabla ya hatua kuchukuliwa dhidi yao.

 

RELATED TOPICS:

Would you like to get published on Standard Media websites? You can now email us breaking news, story ideas, human interest articles or interesting videos on: [email protected]

RECOMMENDED