Standard Digital News - Radio Maisha | Haki za Mashoga
Kipindi cha sasa Safari

Haki za Mashoga

Wito umetolewa kwa vyombo vya habari kuangazia kwa usawa taarifa zinazohusu wasenge na wasagaji. Akitoa wito huo, afisa anayeshughulikia uratibu wa mipango katika shirika la ICJ tawi la Kenya Judy Gitau amesema kuwa kwa kiwango fulani, vyombo vya habari vimechangia katika kuongezeka kwa visa vya kubaguliwa kwa wanaoshiriki ndoa ya jinsia moja. Aidha, afisa huyo amesema kuwa mikakati imebuniwa na mashirika mbali mbali ya kupigania haki za kibinadam ambayo itawahusisha wanasiasa, vyombo vya habari na taasisi zinginezo kuuhamasisha umma kuhusu haki za wanaoshiriki ndoa ya jinsia moja. Gitau alikuwa akizungumza katika hafla ya kuangazia haki za mashoga na wasagaji iliyofanyika katika ubalozi wa Marekani hapa Nairobi.
Comment Policy
comments powered by Disqus