KUPPET chatishia kuitisha mgomo wa walimu

Na ,Suleiman Yeri

KUPPET chatishia kuitisha mgomo wa walimu iwapo shule hazitafungwa kutokana na kukithiri kwa visa vya moto shuleni


Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Kadri, KUPPET kimetishia kuitisha mgomo wa walimu iwapo shule hazitafungwa kutokana na kukithiri kwa visa vya moto shuleni. Chama hicho kimempa Waziri wa Elimu, Fred Matiang'i makataa ya siku saba kuzingatia wito huo.
KUPPET aidha inataka walimu wanaozuiliwa kwa kuhusishwa na moto shuleni kuachiliwa mara moja.
Wito wa kufungwa kwa shule vilevile umetolewa na Muungano wa CORD. Kwenye kikao na wanahabari katika majengo ya bunge kilichoongozwa na Naibu Kiongozi wa Wachache katika Seneti, Moses Wetangula, Seneta Omar Hassan na Mwenyekiti wa ODM John Mbadi, muungano huo umemlaumu Waziri Matiang'i kwa kuteketeza sheria mpya bila kuwashirikisha washikadau wote, suala wanalosema limechangia hali inayoshuhudiwa kwa sasa.
Aidha wanataka suala la kuteketezwa kwa majengo shuleni kutangazwa kuwa janga la taifa.