OUKO AFIKA MBELE YA KAMATI

NA CARREN OMAE

Mhasibu Mkuu wa Serikali Edward Ouko amefika mbele ya Kamati ya fedha ya bunge la Kitaifa kujitetea dhidi ya hoja ya kutaka kumng'atua ofisini. Ouko ameandamana na wakili wake Otiende Omollo, ambaye anatoa maelezo mbele ya kamati kwa niaba ya mhasibu Mkuu huyo.

Licha ya kamati hiyo kusisitiza kwamba Ouko anafaa kujibu maswali hayo binafsi, wakili wake amesisitiza kwamba ana haki akiwa wakili wa afisa wa serikali kumwakilisha.

Aidha Kamati hiyo imemhakikishia kwamba uchunguzi dhidi yake utafanywa kkwa mujibu wa utaratibu katika katiba.

 

Related Topics