ARSENAL NA CHELSEA MBINGU YA SABA!

Na Stephen Mukangai

KLABU ya Arsenal imepanda hadi nafasi ya pili kwenye jedwali la ligi ya premier baada ya kuitandika Burnley magoli 2-1 katika pambano kali lililoandaliwa uwanjani Emirates mwishoni mwa Juma. 

Wachezaji Mustafi na Alexis Sanchez walipachika wavuni goli moja kila mmoja. 

Arsenal ilimaliza mchezo ikiwa na wachezaji kumi uwanjani baada ya Granit Xhaka kuoneshwa kadi nyekundu. 
Vilevile kocha Arsene Wenger alitimuliwa uwanjani kwa kosa la kumsukuma machi komisari.
Kwenye matokeo mengine Chelsea iliinyuka Hull City magoli 2-0. Wachezaji Diego Costa na Garry Cahili walipachika wavuni goli moja kila mmoja.
 

Related Topics

ARSENAL CHELSEA