''Msiwe na wasiwasi kuhusu umiliki wa ardhi zenu'' Serikali yawaambia wakenya

Na Sophia Chinyezi
Serikali imewashauri Wakenya kutokuwa na wasiwasi kuhusu uhalali wa mikopo, idhini ya kumiliki ardhi kwa muda na hati miliki zilizotolewa na serikali ya Jubilee baada ya mwaka 2013, akisema agizo lililotolewa na mahakama hivi majuzi imesitishwa kwa mwaka mmoja.
Waziri wa Ardhi Jacob Kaimenyi amesema ripoti zinazotolewa na vyombo vya habari zina makosa kwa kuwa Mahakama Kuu iliipa serikali mwaka mmoja kuthibitisha hati miliki zote kufuatia ushauri wa Tume ya Ardhi Nchini NLC, maoni ya wananchi na idhini ya Bunge, ili zifanywe kuendeana na sheria.
Kadhalika Kaimenyi amesema wamebuni jopokazi kuangazia kanuni zilizopo kwa muda wa miezi miwili, ambapo marekebisho ya sheria za ardhi iliyofanyiwa marekebisho itakapotekelezwa, ilivyoagizwa na mahakama.
Vilevile ameuhakikishia umma kwamba wizara yake itahakikisha kwamba sheria zilizopo zinakamilishwa na kuwasilishwa Bungeni ili kudihiniswa katika kipindi kilichotolewa na mahakama ili kuzuia vyeti hivyo kufutiliwa mbali.