Benki ya Co-operative yatia sheria mpya kuhusu riba

Na, Mike Nyagwoka

Benki ya Cooperative imekuwa ya kwanza kutangaza viwango vipya vya riba kufuatia sheria mpya ya kudhibiti riba ya mikopo inayotolewa na benki. Afisa Mkuu Mtendaji wa benki hiyo, Gideon Muriuki amesema Cooperative haitawatoza wateja wake riba inayopita asilimia 14.5  kuanzia sasa.
Haya yanajiri huku chama cha wahasibu, ICPAK  kikiwashauri washikadau katika sekta nzima ya benki kufanya mabadiliko kuhusu viwango vya riba. Aidha chama hicho kupitia Mwenyekiti wake, Fernades Barasa kimeitaka serikali kuandaa sheria itakayodhibiti mashirika mengine ya kutoa mikopo kama vile vyama vya ushirika na watu binafsi kwa Kiingereza Shylocks.