27th January, 2022
Siku chache baada ya KTN News kuangazia masaibu ya Afisa wa Polisi Wycliffe Nyonyoki ambaye alidai amekuwa akihudumu katika kituo cha polisi bila mshahara kwa miaka mitatu na mshahara nusu kwa miaka kumi na saba iliyopita, msemaji wa polisi Bruno Shioso amepinga madai ya afisa huyo wa polisi na kusema licha ya mahakama ilikuwa imetupilia mbali makosa yake jopo la uchunguzi la polisi lilimpata na makosa na kumtimua.