18th June, 2021
Katibu mkuu wa chama cha jubilee Raphael Tuju amethibitisha kwamba kuna mpango wa chama hicho kuungana na ODM kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao. Tuju anasema siku chache zijazo vyama hivyo viwili vitaweka sahihi makubaliano hayo huku vikilenga kuteua mgombea mmoja wa urais kwa uchaguzi mkuu wa 2022.