5th June, 2020
Viongozi kutoka maeneo ya magharibi ya kenya wamezitaka jamii zinazozozana katika mpaka wa kaunti za Nandi na Kakamega kusitisha uhasama wa kijamii ambao umesababisha vita baina ya jamii mbili, huku jitihada za suluhu likiendelezwa na wazee wajamii mpakani humo. Wakizungumza huko Kakamega, waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa amesema kuna haja ya jamii zinazohasimiana kukaa kitako na kutatua tatizo hilo, wakati wazee wa jamii wameonekana kukutana na kuhubiri amani katika vikao vyao kwa maslahi ya jamii.