29th May, 2020
Takriban watu thelathini na wanane kutoka kisumu walikamatwa na kufikishwa mahakamani baada ya kukiuka masharti ya serikali ya kukabiliana na korona kwa kutovalia maski na kutozingatia umbali uliowekwa. Waathiriwa walikamatwa katika barabara za mtaa wa Milimani na Tom Mboya jana asubuhi. Walifika mahakamani wakiwa wamevalia mavazi yao ya mazoezi na wakashtakiwa kwa kukiuka kanuni zilizotolewa na waziri wa afya kuhusu sheria ya Afya ya umma. Hakimu mkuu mwandamizi Robbinson Ondieki aliwapata na hatia lakini watoto waliachiliwa na kuonywa wasirudie kukiuka kanuni za kukabiliana na msambao wa virusi vya korona nchini