Mgomo wa Madaktari Kakamega kuanza tarehe 1 Februari, wanadai mkataba wao haujazingitiwa

KTN News Jan 31,2020


View More on Leo Mashinani

Mgomo wa madaktari katika kaunti ya kakamega utango'a nanga rasmi usiku wa kuamkia tarehe Mosi mwezi Februari baada ya wizara ya Afya katika Kaunti ya Kakamega kukataa kutekeleza matakwa ya Muungano wa Madaktari kwa siku 21 walizowapa. Antony Akoto Mwenyekiti wa Muungano huo ametoa ilani hiyo ya mgomo kwa madai kuwa siku 21 walizoipa Wizara ya Afya kutekeleza matakwa yao imefika bila jawabu kutoka kwa wahusika Gofrey Githenji anasema kuwa hamna swala jipya wanalodai ila ni kutekelezwa kwa matakwa waliyoahidiwa na Wizara ya Afya walipotaka kuelekea mgomoni mwaka jana .Juhudi za Muungano huo kufikia Afisi za Wizara wa Afya ziligonga mwamba huku viongozi hawa wakimtaka Gavana Wycliff Oparanya kuwatimua maafisa hao wanaodai wanalenga kukandamiza Ajenda ya Gavana Oparanya.