Mwili wa mwanamke aliyekuwa mfanyikazi wa shamba la maua wapatikana Naivasha

KTN News Jan 10,2020


View More on Leo Mashinani

Siku Kumi Za Kumtafuta Mama Mmoja Wa Watoto Watatu Ziliisha Na Huzuni Na Majonzi Baada Ya Mwili Wake Ulioharibika Kupita Kiasi Kupatikana Ukiwa Umezikwa Kwenye Kaburi Moja Katika Mtaa Wa Karagita Eneo La Naivasha. Mwili Wa Mfanyakazi Huyo Wa Shamba La Maua Ulipatikana Na Mguu Mmoja Huku Jicho Moja Likiwa Halipo. Mwanamke Huyo Kwa Jina Nancy Wangui Alipotea Siku Ya Mwaka Mpya Baada Ya Kutoka Nyumbani Kwake Mwendo Wa Saa Kumi Unusu Alfajiri Kueleka Kazini Kwenye Mojawepo Wa Mashamba Ya Maua Alikokuwa Akifanya Kazi.