Afisa wa polisi na mwanafunzi wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa pombe Thika | MBIU YA KTN

KTN News Jan 07,2020


View More on KTN Mbiu

Afisa mmoja wa polisi anayehudumu katika kituo cha polisi cha Thika amefikishwa mahakamani pamoja na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha Kenyatta kwa tuhuma za wizi. Afisa huyo wa kike Ansatazia Wanjiru na mwanafunzi huyo Ben Kamau walifikishwa mbele ya hakimu Oscar Wanyanga na kusomewa mashtaka matatu kila mmoja kwamba kati ya tarehe 15 Novemba mwaka jana na mwezi huu wa Januari tarehe 4, walishirkiana kuvunja lango la jengo la vileo na kuiba bidhaa zinazokadiriwa kugharimu shilingi milioni tatu. Walikanusha mashtaka dhidi yao na mahakama itatoa uamuzi wa kuwaachilia kwa dhamana au la.