1st January, 2020
Katibu mkuu wamuungano wa vyama vya wafanyakazi, COTU, Francis Atwoli amesisitiza lazima mkutano ulioratibiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu wa Januari mjini Kakamega utafanyika, akipinga madai ya baadhi ya viongozi wa jamii ya Magharibi kuwa mkutano huo ni wa kumteua atakayegombea kiti cha urais kwa niaba ya jamii hiyo. Atwoli anasema mkutano huo ni wa kuunga mkono mapendekezo ya ripoti ya BBI wala si siasa