16th December, 2019
Ni Rasmi Kuwa Mtihani Wa Kidato Cha Nne Ksce Mwaka Huu Wa 2019 Umemamilizika Kusahihishwa Na Hata Kutathminiwa. Matokeo Yanasubiriwa Kutangazwa Wakati Wowote Kutoka Sasa.Walimu Na Maafisa Husika Walipaswa Kuusahihisha Mtihani Huo Kati Ya Tarehe 28 Mwezi Novemba Siku Moja Tu Baada Ya Kukamilika Kwa Mtihani Mwa Mwisho Na Tarehe 12 Disemba. Duru Zinaarifu Kuwa Shughuli Hiyo Ilikamilika Kabla Ya Siku Hiyo Na Sasa Na Yanasubiriwa Kuwekwa Wazi Kwa Umma. Waziri Wa Elimu Prof. George Magoha Anasubiriwa Kuyatangaza Matokeo Hayo Kunako Muda Wowote Na Kama Alivyotangaza Kuwa Wazazi Watajua Matokeo Kabla Ya Sherehe Za Krismasi Na Mwaka Mpya Tayari Taharuki Na Imetanda Kote Nchini. Walimu, Wanafunzi, Wazazi Na Walezi Wakiyasubiri Matokeo Hayo Kwa Hamu Mno Japo Kwa Hisia Mseto.