Hali ya uzuni imetanda Busia baada ya mchimba mchanga kuzikwa hai

KTN News Dec 11,2019


View More on KTN Leo

         Hali ya huzuni imewakumba wenyeji wa kijiji cha mudembi huko Budalangi kaunti ya Busia baada ya mchimba mchanga mmoja kuzikwa akiwa hai kwenye chimbo alimokuwa akifanya kazi  Kulingana na wenyeji eneo hilo mwendazake aliyejulikana kwa jina Klegan Otieno mwenye umri wa miaka 7 alikumbana na kifo akiwa na wenzake 3 waliokuwa wakichimba mchanga huku wenzake wakiponea kwa majeraha mabaya Ni mkasa wa pili kutokea chini ya wiki mbili na sasa wanataka serikali kutoa hamasisho ya namna ya kuendesha shughuli hiyo. Mwili wa mwendazake ulipelekewa katika hifadhi ya maiti katika hospitali ya Port Victoria.