×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mzozo wa uchukuzi wajitokeza huku wenye magairi aina ya Probox wakilaumiwa

10th December, 2019

Shughuli za chukuzi wa umma katika eneo la Mbooni, kaunti ya Makueni zilitatizika  baada ya madereva wa matatu, kuandamana wakidai kuwa wenzao walio na magari ya Probox wanawanyanganya biashara ya uchukuzi ilhali hawana kibali cha kuhuduma katika sekta hiyo. Wahudumu hao wa matatu ni wale hufanya uchukuzi katika barabara za Kikima kuelekea ?Tawa?Masii?Machakos hadi Nairobi na vile vile wengine wanaohudumu kuelekea Wote?Makindu na Kibwezi.

 Eneo la Mbooni lina magari mengi ya Probox ambayo yanapatikana katika kila barabara huku madereva wakidaiwa kukiuka sheria za trafiki kwa kubeba watu wengi kupita kiasi hadi sehemu ya nyuma ya gari kinyume cha sheria. Mgomo huo uliwafanya abiria wengi wanaosafiri kwenda sehemu mbali mbali  kutatizika huku wengi wao ambao walikuwa wakielekea maeneo ya karibu wakilazimika kutumia pikipiki.

.
RELATED VIDEOS