Zaidi ya familia 150 zinaishi bila makao baada ya nyumba zao kufurika maji eneo bunge la Nyatike
10th December, 2019
Zaidi ya familia 150 katika eneo la nyatike kaunti ya Migori sasa zinaishi bila makao baada ya nyumba zao kufurika maji kutokana na mvua kubwa inayoshuhudiwa eneo hilo. Kijiji kilichoathirika zaidi ni cha Sagama ambacho inadaiwa kimeathiriwa na maji ya mpango wa unyunyizaji maji mashamba wa Lower Kuja.Gavana wa eneo hilo Okoth Obado alizuru waathiriwa na kutoa wito kwa serikali ya kitaifa kuingilia kati na kuwatafutia makao mbadala wahanga wote. Alizungumza akiwa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani kwa ndani ya Agenga ambapo zaidi ya watu 500 wanaishi