10th December, 2019
Mashindano ya bara ya mchezo wa sataranji almaarufu chess kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16 yanakamilika hii leo hapa jijini nairobi. Uganda ingali inaongoza msimamo licha ya kulazwa na tanzania katika raundi ya sita mapema leo huku sasa raundi moja pekee ikisalia mashindano hayo kukamilika. Mataifa mengine yanayoshiriki mashindano hayo kando na uganda ni wenyeji kenya, tanzania na sudan kusini.