Sonko alazwa katika hospitali ya Kenyatta baada ya kuugua usiku wa kuamkia leo | MBIU YA KTN

KTN News Dec 10,2019


View More on KTN Mbiu

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amelazwa katika hospitali ya kitaifa ya kenyatta baada ya kuugua usiku wa kuamia leo  akiwa katika gereza la kamiti.hapo jana  hakimu mkuu wa mahakama ya milimani douglas ogoti alimruhusu sonko kutafuta matibabu. Sonko pamoja na washukiwa wengine walikanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yao na wataendelea kuzuiliwa hadi hapo kesho kesi ya kutaka kupewa dhamana itakapoamuliwa. Mawakili wa sonko walitaka mteja wao kupewa dhamana kwa msingi kwamba ni mgonjwa na atahitaji matibabu. Hata hivyo upande wa mashtaka ulikataa ombi la sonko kwa msingi kwamba huenda akahepa.