10th December, 2019
Vita Dhidi Ya Ukeketaji Wa Wanawake Vimepata Muinuko Baada Ya Viongozi Wa Siasa Kuraiwa Kutoa Msaada Wa Kifedha Kwa Wanawake Wataalam Wanaoendeleza Mila Hiyo Mbovu Ili Kuwaruhusu Kutafuta Njia Mbadala Za Kujipa Riziki Na Kukomesha Ukeketaji Kwenye Kaunti 22 Zilizoshamiri Mila Hiyo. Wakiongozwa Na Afisa Msimamizi Katika Wizara Ya Huduma Za Umma Na Jinsia Rachel Shebesh, Baadhi Ya Washikadau Wametaja Kusikitishwa Na Ongezeko La Visa Vya Ukeketaji Miongoni Mwa Wanawake Licha Ya Juhudi Za Kitaifa Kukomesha Mila Hizo Mbovu.