10th December, 2019
Vuta Ni Kuvute Ya Kisiasa Kati Ya Gavana Wa Kiambu Ferdinand Waititu Na Naibu Wake James Nyoro Inatarajiwa Kurejea Tena Kwenye Bunge La Kaunti Ya Kiambu Adhuhuri Ya Leo Huku Viongozi Hao Wote Wawili Wakizingira Na Masaibu Ya Kutaka Kung’atuliwa Madarakani. Mswada Dhidi Ya Waititu Umependekezwa Na Mwakilishi Wadi Wa Ndenderu Solomon Kinuthia Huku Ule Dhidi Ya Naibu Wake Ukiwasilishwa Na Mwakilishi Wadi Wa Weteithie Julius Macharia. Wapinzani Wa Waititu Wanasema Anapaswa Kungatuliwa Kwa Tuhuma Za Ufisadi Huku Wanaopinga Nyoro Wakisema Kwamba Hatoshi Mboga Kusimamia Masuala Ya Kaunti Ya Kiambu .